Ufunuo Aliopewa kwa Yohane
Mimi Yohane nayaandikia makanisa yaliyoko mkoani Asia. Nawatakieni
neema na amani kutoka kwake yeye aliyeko, aliyekuwako na anayekuja; na
kutoka kwa roho saba walio mbele ya kiti chake cha enzi,
na kutoka kwa-Yesu Kristo, shahidi mwaminifu, wa kwanza kufufuliwa
kutoka wafu, na ambaye ni mtawala wa wafalme wa dunia.
Salamu kwa makanisa saba
Yeye anatupenda, na kwa damu yake ametufungua kutoka vifungo vya
dhambi zetu,
akatufanya sisi kuwa ufalme wa makuhani, tumtumikie Mungu, Baba
yake. Kwake Yesu Kristo uwe utukufu na nguvu, milele na milele! Amina.
Tazama! Anakuja katika mawingu! Kila mtu atamwona, hata wale
waliomchoma. Makabila yote duniani yataomboleza juu yake. Naam! Amina.
"Mimi ni Alfa na Omega," asema Bwana Mungu Mwenye Uwezo,
aliyeko, aliyekuwako na anayekuja.
Kwa malaika wa kanisa la Laodikea andika hivi:
- Huu ndio ujumbe kutoka kwake yeye aitwaye Amina. Yeye ni shahidi
mwaminifu na wa kweli, ambaye ni chanzo cha viumbe vyote alivyoumba
Mungu.
- Nayajua mambo yako yote! Najua kwamba wewe si baridi wala si
moto. Afadhali ungekuwa kimojawapo: baridi au moto.
- Basi, kwa kuwa hali yako ni vuguvugu, si baridi wala si moto,
nitakutapika!
- Wewe unajisema, Mimi ni tajiri; ninajitosheleza, sina haja ya
kitu chochote.
- Kumbe, hujui kwamba wewe ni mnyonge, unahitaji
kuhurumiwa, maskini, kipofu tena uko uchi!
- Nakushauri ununue kwangu dhahabu iliyosafishwa kwa moto upate kuwa
tajiri kweli. Tena afadhali ununue pia vazi jeupe, uvae na
kufunika aibu ya uchi wako.
- Nunua pia mafuta ukapake machoni pako upate kuona. Mimi ndiye
mwenye kumwonya na kumrudi yeyote ninayempenda. Kwa hiyo kaza
moyo, achana na dhambi zako.
- Sikiliza! Mimi nasimama mlangoni na kubisha hodi. Mtu akisikia
sauti yangu na kufungua mlango, nitaingia nyumbani kwake na kula chakula
pamoja naye, naye atakula pamoja nami.
Tarumbeta
Kisha wale malaika saba wenye tarumbeta saba wakajiweka tayari
kupiga mbiu ya mgambo.
ic
Malaika...
Malaika wa kwanza akapiga tarumbeta yake. Mchanganyiko wa mvua ya mawe
na moto, pamoja na damu, ukamwagwa juu ya nchi. Theluthi moja ya nchi
ikaungua, theluthi moja ya Miti ikaungua, na majani yote
mabichi yakaungua.
- Malaika wa pili akapiga tarumbeta yake.
- Na kitu kama mlima mkubwa
unaowaka moto ukatupwa baharini. Theluthi moja ya bahari ikawa damu,
theluthi moja ya viumbe vya baharini vikafa na theluthi moja ya
meli zikaharibiwa.
- Kisha malaika wa tatu akapiga tarumbeta yake.
- Na nyota kubwa
ikiwaka kama bonge la moto, ikaanguka kutoka mbinguni, na kutua juu ya
theluthi moja ya mito na chemchemi za maji.
- Nyota hiyo inaitwa "Uchungu."
- Basi, theluthi moja ya maji
yakawa machungu; watu wengi wakafa kutokana na maji hayo, kwa sababu
yaligeuka kuwa machungu.
- Kisha malaika wa nne akapiga tarumbeta yake.
- Ndipo theluthi moja
ya jua, ya mwezi na ya nyota ikapata pigo; hata mwangaza ukapoteza
theluthi moja ya mng'ao wake. Theluthi moja ya mchana ikakosa mwanga,
hali kadhalika na theluthi moja ya usiku.
Kisha nikatazama, nikasikia tai akiruka juu kabisa angani anasema
kwa sauti kubwa, "Ole, ole, ole kwa wanaoishi duniani wakati malaika
watatu waliobaki watakapopiga tarumbeta zao!"
Kisha malaika wa tano akapiga tarumbeta yake. Nami nikaona nyota
iliyokuwa imeanguka juu ya nchi kutoka mbinguni. Nayo ikapewa ufunguo
wa shimo la Kuzimu.
Basi, nyota hiyo ikafungua shimo la Kuzimu, kukatoka moshi wa
tanuru kubwa. Jua na anga vikatiwa giza kwa moshi huo wa Kuzimu.
Nzige wakatoka katika moshi huo, wakaingia duniani wakapewa nguvu
kama ya ng'e.
Wakaamrishwa wasiharibu nyasi za nchi wala majani wala miti
oyote, bali wawaharibu wale tu ambao hawakupigwa mhuri wa Mungu katika
paji la uso.
Nzige hao hawakuruhusiwa kuwaua watu, ila kuwatesa tu kwa muda wa
miezi mitano.
Maumivu?
Maumivu watakayosababisha ni kama maumivu yanayompata mtu
wakati anapoumwa na ng'e.
- Muda huo watu watatafuta kifo
- lakini hawatakipata;
- watatamani kufa
- lakini kifo kitawakimbia.
- Kwa kuonekana, nzige
- hao walikuwa
- kama farasi waliowekwa
- tayari
- Kwa vita.
- Juu ya vichwa vyao walikuwa
- na taji zilizo kama za
- dhahabu, na
- hao walikuwa
- kama farasi waliowekwa
- tayari
- nyuso zao zilikuwa
- kama za binadamu.
Nywele zao...
Nywele zao zilikuwa kama nywele za wanawake, na meno yao yalikuwa
kama meno ya simba.
Vifua vyao...
Vifua vyao vilikuwa vimefunikwa kitu kama ngao ya chuma. Sauti ya
mabawa yao ilikuwa kama sauti ya msafara wa magari ya farasi wengi
wanaokimbilia vitani.
Walikuwa na mikia...
Walikuwa na mikia na miiba kama ng'e, na kwa mikia hiyo, walikuwa
na nguvu ya kuwadhuru watu kwa muda wa miezi mitano. Tena wanaye
mfalme anayewatawala, naye ndiye malaika wa kuzimu; jina lake kwa
Kiebrania ni Abadoni, na kwa Kigiriki
ni Apolioni, yaani mwangamizi.
Sean M. Burke, 1 May 1995